Na Elder Robert D. Hales
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawil
Mengi
yameandikwa na kusemwa kuhusu kizazi cha leo cha vijana wazima. Utafiti
unaonyesha kwamba wengi wanapinga dini yenye utaratibu. Wengi wana
madeni na hawana ajira. Wengi wao wanapenda wazo
la ndoa, lakini wengi wanaogopa kuchukua hatua hiyo. Idadi
inayoongezeka haitaki watoto. Bila injili na mwongozo wenye maongozi,
Wengi wanazunguka-zunguka katika njia ngeni na wanapoteza njia zao.
Kwa
bahati nzuri, vijana wazima waumini wa Kanisa wamebakia nyuma katika
mielekeo hii inayosumbua, kwa kiasi, kwa sababu tumebarikiwa na mpango
wa injili. Mpango ule unajumuisha kushikilia kwa nguvu fimbo ya
chuma—kujishikilia kwenye neno la Mungu na neno la manabii Wake.
Tutashikilia fimbo ambayo inatuelekeza kurudi kwake? Sasa ni “siku ya
kuchagua”1 kwetu sote.
Nilipokuwa
mvulana, wakati nilipokuwa karibu kufanya uchaguzi ambao nilikuwa
sijaukagua vyema, baba yangu wakati mwingine angesema, “Robert, kuwa
makini na ufanye kile unachojua ni sahihi! Ninyi mmeshapitia hayo.
Katika roho ya mazungumzo yake ya wazi, ningependa kusema hususani kwenu
vijana—vijana waungwana—vijana wazima wetu waungwana, kwani “roho yangu
hufurahia katika uwazi ... ili kwamba [tuweze] kujifunza.”2
Mnaishi
katika kipindi cha muda muhimu cha maisha yenu. Chaguzi
mnazofanya—misheni, elimu, ndoa, ajira na huduma katika
Kanisa—zitawaletea uzoefu milele. Hii inamaanisha siku zote lazima muwe
mnalenga mbele—mkilenga siku zijazo.
Kama
rubani katika Jeshi la Anga, nilijifundisha kanuni hii: kamwe usiruke
kwa makusudi katika mvua ya radi. (Mimi sitakwambia jinsi nilivyogudua
hayo.) Badala yake izunguke, chukua njia ingine, au ngoja dhoruba iishe
kabla ya kutua.
Wapendwa
vijana wazima, ndugu na akina dada, Nataka kuwasaidia “kuruka kwa
usahihi” wakati wa dhoruba za siku za mwisho zinapotanda. Ninyi ni
marubani. Wajibu wenu ni kufikiri kuhusu matokeo ya kila uchaguzi.
Jiulizeni wenyewe, "Kama nikifanya uchaguzi huu, ni kitu ngani kibaya
sana ambacho kinaweza kutokea?” Uchaguzi wenu sahihi utawasaidia
msichepuke kutoka kwenye mwelekeo sahihi.
Fikirieni
kuhusu hilo: Kama mtachagua kutokunywa pombe, hamtakuwa mlevi! Kama
kamwe hamtachagua kuwa na madeni, mtaepuka uwezekano wa kufilisika!
Mojawapo
ya madhumumi ya maandiko ni kutuonyesha jinsi watu wenye haki wanajibu
majaribu na uovu. Kwa kifupi, Yaepuke! Yusufu alimkimbia mke wa Potifa.3 Lehi alichukuwa familia yake na waliondoka Yerusalemu.4 Mariamu na Yusufu walikimbilia Misri kutoroka njama ovu ya Herode.5
Katika kila mfano, Baba wa Mbinguni aliwatahadharisha waumini hawa.
Vilevile, Yeye atatusaidia sisi kujua kama tupigane, tukimbie, au
kukubali hali zetu zinazobadilika. Yeye atanena kwetu kupitia sala,
wakati tunaposali, tutakuwa na Roho Mtakatifu, ambaye atatuongoza. Tuna
maandiko, mafundisho ya manabii wanaoishi, baraka za Baba mkuu, ushauri
wa kutia moyo wa wazazi na viongozi wa ukuhani na makundi saidizi, na
zaidi ya hao, sauti ndogo tulivu ya Roho.
Bwana daima ataweka ahadi Yake: “Nitakuongoza siku zote.”6 Swali pekee ni, tutajiachia wenyewe tuongozwe? Tutasikia sauti Yake na sauti za watumishi Wake?
Ninashuhudia kwamba kama upo hapo kwa ajili ya Bwana, Yeye atakuwepo kwa ajili yako.7
Kama unampenda Yeye na kutii amri Zake, utakuwa na Roho Wake apate kuwa
pamoja nawe na kukuongoza. “Weka imani yako katika Roho yule ambaye
anakuongoza kufanya mema. ... Kwa hii tutajua vitu vyote ... kuhusu vitu
vya haki.”8
Pamoja na kanuni hizo kama msingi, naweza kuwapeni ushauri kiasi wa kiutendaji?
Wengi
wa kizazi chenu wanakabiliwa na madeni makubwa mno. Wakati nilipokuwa
kijana, Rais wa kigingi changu alikuwa Mkurugenzi wa banki ya kitega
uchumi kwenye Wall Street. Alinifundisha, “Wewe ni tajiri kama unaweza
kuishi kwa furaha kwa njia ambayo unatumia kidogo kuliko kipato chako.
Unaweza kufanya vipi? Lipa zaka yako na kisha weka akiba! Wakati
unachuma zaidi, weka akiba zaidi. Usishindane na wengine kuwa na vitu
vya gharama. Usinunue kile usichoweza kukimudu.
Vijana
wengi katika ulimwengu wanaingia kwenye madeni kupata elimu na baadaye
wanakuta gharama ya shule ni kubwa mno kuliko wanavyoweza kulipa. Tafuta
msaada wa masomo, mikopo isiyo na riba. Pata ajira ya muda, na kama
inawezekana, ikusaidie kulipa gharama yako mwenyewe. Hii itahitaji
dhabihu kiasi, lakini itawasaidia kufanikiwa.
Elimu
hukutayarisha kwa nafasi nzuri za ajira. Huwaweka kwenye nafasi nzuri
ya kuhudumu na kuwabariki wale walio karibu nanyi. Itawaweka kwenye njia
kujifunza ya maisha yote. Itawaimarisha kupigana dhidi ya upumbavu na
makosa. Kama vile Joseph Smith alivyofunza: “Elimu huondosha giza, wasi
wasi na shaka; kwa haya hayawezi kuwepo pale elimu ilipo. ... Katika
elimu kuna uwezo.”9 “Lakini kuelimika ni vyema ikiwa watatii mawaidha ya Mungu.”10 Elimu itawatayarisha ninyi kwa kile kilicho mbele, ikijumuisha ndoa.
Tena,
naomba niseme wazi kabisa? Njia ile inayoelekea kwenye ndoa hupitia
upeo unaoitwa miadi! Miadi ni nafasi ya mazungumzo marefu. Wakati
mnafanya miadi, jifunze kila kitu kuhusu nyote wenyewe. Jifahamisheni na
familia inapowezekana. Je! Malengo yenu yanambatana? Je! Mnashiriki
hisia sawa kuhusu maandiko, Mwokozi, ukuhani, hekalu, ulezi, wito wa
Kanisani, na kuwahudumia wengine? Je! Mshaangliana kwa makini
mnapokabiliwa shida, mjibizo wa fanaka, ushinde, kujizuia ghadhabu, na
kukabilia na vikwazo? Je! Yule anayefanya miadi naye uvuruga watu ama
huwajenga? Je! Mtazamo na lugha na mwenendo wake ndiyo vile ungependa
kuishi navyo kila siku?
Baada ya hayo yote, hakuna kati yetu anayeowa mtu aliye kamili; tunaoa mwenye uwezo.
Ndoa sahihi si tu ile inayohusu nini tunataka; ni kuhusu nini
anachotaka na kile—yule ambaye atakuwa mwenzi wangu—anataka na anahitaji
mimi niwe.
Tukisema
kwa uwazi, tafadhali usiwe na miadi katika umri wako wote wa miaka ya
20 ili tu “ujifurahishe” hivyo ukachelewesha ndoa kwa ajili ya maslahi
mengine. Kwa nini?” Kwa sababu miadi na ndoa si kikomo cha safari zetu.
Ni lango la kule hatimaye tunataka kwenda. “Kwa hiyo mwanaume atamwacha
baba yake na mama yake, na atashikamana kwa mke wake.”11
Jukumu
lako sasa ni kuwa mstahiki kwa mtu unayetaka kumwoa. Kama unataka kuoa
mwenye uchangamfu, anayevutia, mwaminifu, mwenye furaha, mchapa kazi,
mtu wa kiroho, basi uwe mtu wa aina hiyo. Kama wewe ni
mtu huyo na hujaoa bado, kuwa na subira. Msubirie Bwana. Nashuhudia
kwamba Bwana anajua hamu zako na anakupenda kwa kujitolea kwako kwa
imani Kwake. Ana mpango kwa ajili yako, iwe ni katika maisha haya ama
yajayo. Silikiliza Roho Wake. “Usitafute kumshauri Bwana, lakini kupokea
ushauri kutoka kwake.”12 Katika maisha haya au yajayo, ahadi zake zitatimizwa. “Kama umejitayarisha hutaogopa.”13
Kama
hauna mali nyingi, usijali. Muumini wa ajabu wa Kanisa majuzi
aliniambia, “Mimi sikuwalea watoto wangu kwa pesa; niliwalea kwa imani.
Kuna ukweli mkuu katika hayo. Anza kufanya imani katika kila sehemu ya
maisha yako. Kama hautafanya hivyo, utaugua kile ninachokiita “imani
nyauka.” Nguvu hasa zinazohitajika kufanya imani yako zitafifia. Kwa
hivyo fanya imani kila siku, na wewe atapata “nguvu kwa nguvu ... wakawa
imara zaidi na imara katika imani ya Kristo.”14
Kuwa
tayari kwa ndoa, hakikisheni kwamba mnastahili kupokea sakramenti na
mnastahili kuwa na sifu ya hekalu. Nendeni hekaluni kila mara. Mhudumu
katika Kanisa. Pamoja na miito ya Kanisa, fuateni mfano wa Mwokozi,
ambaye kwa urahisi, “aliendelea kufanya mema.”15
Sasa,
mnaweza kuwa na maswali ya dhati kuhusu chaguzi za huko mbele. Katika
miaka ya ujana wangu, nilitafuta ushauri kutoka kwa wazazi wangu na
kutoka kwa washauri waaminifu wanaoaminika. Mmoja alikuwa mwenye
ukuhani; mwingine alikuwa mwalimu ambaye aliniamini. Wote waliniambia,
“Kama unataka ushauri wangu, uwe tayari kuukubali. Mimi nilielewa hiyo
ilimaanisha nini. Kwa maombi chagua wanasihi ambao wana usimamizi wa
kweli kuhusu ufanisi wako wa kiroho. Uwe mwangalifu kuhusu kuchukuwa
ushauri kutoka kwa rika lako. Kama unataka zaidi ya uliyonayo sasa,
angalia juu, siyo kando kando!16
Kumbuka, hakuna anayeweza kufikia juu kwa niaba yenu. Bali imani yenu tu na maombi yatasababisha nyinyi kuwa na mabadiliko makubwa ya moyo. Uamuzi wenu
tu kuwa watiifu unaweza kubadili maisha yenu. Kwa sababu ya dhabihu ya
upatanisho ya Mwokozi kwa ajili yako, uwezo upo ndani yako.17 Una wakala wako, una ushuhuda thabiti kama wewe ni mtiifu, na unaweza kumfuata Roho ambaye hukuongoza.
Hivi
majuzi, kijana mtengeneza filamu alisema alihisi alikuwa sehemu ya
“kizazi cha wapotevu”—kizazi “kinachotafuta matumaini na shangwe na
ukamilifu, lakini kutafuta katika sehemu zote mbaya na kwa njia mbaya.”18
Katika
fumbo la Mwokozi la mwana mpotevu, mwana alikuwa na baraka nyingi
zikimsubiri, lakini kabla hajazidai, ilibidi angalie kwa makini maisha
yake, chaguo zake, na hali zake. Muujiza ambao ulitokea baadaye
umeelezewa katika maandiko kwa kishazi rahisi: “Alipozingatia moyoni
mwake.”19
Acha niwatie moyo mzingatie moyoni mwenu? Katika Kanisa, wakati maamuzi
ya muhimu lazima yafanywe, kila mara tunakuwa na mikutano ya baraza.
Mikutano ya baraza ya familia inatumikia azma sawa. Mnaweza kutaka
kuendesha kile nitaita “baraza binafsi.” Tumia muda kiasi peke yako.
Fikiria kuhusu mambo yaliyo mbele. Jiulize: “Ni sehemu gani za maisha
yangu ninazohitaji kuimarishwa ili kwamba niweze kuwaimarisha wengine?
Wapi nataka niwe wapi mwaka mmoja kutoka sasa? Miaka miwili kutoka sasa?
Ni chaguzi gani ninazohitaji kufanya kufika hapo?” Kumbuka tu, wewe
ndiye rubani, na ndiyo unayeshikilia usukani. Ninashuhudia kwamba
unapojitambua, Baba yako wa Mbinguni atakuja kwako. Kwa mikono ya
kufariji ya Roho Yake Mtakatifu, Yeye atakuongoza.
Ninatoa
ushuhuda wangu kwamba Mungu yu hai. Ninatoa ushuhuda wangu maalumu
kwamba Mwokozi anawependa. “Je, si lazima sisi tuendelee katika kazi hii
[Yake iliyo kuu]? Twende mbele na siyo nyuma.”20
Mnapomfuata Yeye, Atawaimarisha na kuwathibitisha. Yeye atawaleta hata
kwenye nyumba yenu ya juu kabisa. Katika jina la Yesu Kristo, amina.