Friday, 22 December 2017

SEMINA YA VIJANA WETU TAREHE 6 BAGAMOYO MAANDALIZI SAFIII

VIONGOZI WA UMMOJA WA VIJANA


Walipotembelea nakuangalia sehemu ambayo semina ya vijana wetu itaenda kufanyika pale Bagamoyo.

Ewe kijana hii semina sio ya kukosa jiandae tarehe 6 sio mbali.


Saturday, 13 May 2017

KKKT USHARIKA WA KITUNDA RELINI TUPO KWENYE KIPINDI CHA HARAMBEE LEO TUMEZINDUA

Ukiwa kama mkristo kazi hii inatuhusu wote natuifanye kwa moyo.
Kwa mkristo yeyote atakayeguzwa na kuchangia harambee ya ujenzi wa nyumba ya Mungu mchango wako fikisha usharikani pia kama upo mbali kwenye hiii kadi kuna namba ya katibu wetu wa usharika unaweza kuwasiliana nae

Wednesday, 8 March 2017

Mambo makuu matatu yanayofanya kanisa kuwa hai

Bwana Yesu asifiwe…
Kanisa halihitaji mambo mengi ili liwe hai kiroho,bali yapo machache ya msingi yenye kulisimamisha kanisa la Bwana. Kupitia mambo hayo matatu tu,basi mambo mengine huzaliwa. Waamini wa leo wamechoka kuendeshwa kwa ibada zisizo hai,wanataka waongozwe na ibada za Roho mtakatifu. Mambo haya matatu ni nguzo katika kanisa la Bwana,ushindi upatikana katika haya matatu,tuyangalie mambo haya kwa ufupi;
01.MWONGOZO WA ROHO MTAKATIFU.
Kati ya jambo kuu la msingi wa kanisa ni kuwepo kwa maongozi ya Roho mtakatifu.Kanisa pasipo Roho mtakatifu basi hilo si kanisa. Kanisa la kweli ni lile lenye kuongozwa na Roho mtakatifu katika kila kitu,Jambo hili ndilo tunaloliona katika kanisa la kwanza la akina Petro. Kanisa la mitume lile la awali kabisa,halikufanya jambo lolote lile pasipo kuongozwa na Roho wa Bwana. Biblia inasema;
” Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu. ” Luka 24:49
Mitume na wanafunzi wa Bwana Yesu,wanaambiwa wasitoke humo Jerusalem,na wasije wakafanya jambo lolote lile mpaka wavikwe uwezo utokao juu- neno ” Uwezo utokao juu ” ni nguvu za Roho mtakatifu,ambao ni maongozi ya Roho wa Bwana. Hii inaonesha kuwa tegemeo lao lote lilikuwa ni kuongozwa na Roho mtakatifu,kwa kupitia huyo Roho mtakatifu tunaona uhai wa kanisa,tunaona ishara na miujiza ikitendeka,tunaona kanisa likitembea na Yesu maana yu hai,ndipo sasa wanatufundisha sisi wa kanisa la leo kwamba kanisa pasipo Roho mtakatifu basi kanisa hilo si kanisa lililo hai.
Tazama hapa tena,mkazo wa kanisa ni ule ule,mitume wanaambiwa hivi;
” Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;
ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache. ” Matendo 1:4-5
Hivyo, kanisa lililo hai linatambulikana kwa kuongozwa na kusimamiwa na Roho mtakatifu pekee,na wala sio kuongozwa na kusimamiwa na mwanadamu awaye yote . Mwanadamu huwa chini ya uongozi wa Roho mtakatifu,lakini mwenye kuleta uhai wa kanisa ni Roho mtakatifu.
02.NENO LA MUNGU.
Kanisa lolote lile lenye uhai ni lile lenye kuhubiri neno la kweli pasipo kupunguza wala kuongeza. Dhambi inastahili kukemewa kabisa katika kanisa kama vile neno la Mungu lisilokumbatia dhambi. Kanisa lolote likikaa katika neno la Mungu basi kanisa hilo ni sawa na kukaa ndani ya Yesu Kristo,biblia ;
” Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.’ ‘ Wakolosai 3:16
Kukaa ndani ya Yesu ni kulijaza neno lake na kulishika,nasi tukikaa ndani yake naye hukaa ndani yetu. Neno la Mungu ni taa ya njia yetu,kwa neno kanisa uwa hai. Ukihitaji kulijua kanisa la kweli ni lile lenye kuhubiri na kufundisha kweli yote. Kanisa la kweli haliwezi kuongozwa na litrujia ya mwanadamu,bali kwa neno la Mungu aliye hai.
Yapo makanisa leo,hayafundishi ile kweli,makanisa ya namna hii hujaa maongozi ya kibinadamu,mbwembwe na hisia za kibinadamu .NK
Mfano mdogo tu ni huu;
Kanisa la kweli haliwezi kutegemea mafuta,chumvi au vitambaa kama ulizi kwa waamini wake. Ulizi wa kweli ni kwa kupitia jina la Yesu Kristo tu,hakuna kingine kinachoweza kumlinda mtu isipokuwa kwa jina hilo.Mtu hatakaswi kwa ibada ya vitambaa,wala mafuta bali hutakaswa kwa neno la Mungu tu. Imeandikwa; ” Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. ” Yoh.17:17,
Yesu anasema tena kwamba ulinzi wa kweli upo katika jina lake tu,na wala ulinzi haupo katika maji,vitambaa,mafuta,mchanga,chumvi kama wengine wafanyavyo leo N.K;
” Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. ” Yoh.17:12
Msingi wa neno la Mungu ndio msingi wa kanisa la Kristo Yesu,Hivyo Neno la Mungu hulifanya kanisa kuwa hai.
03.MAOMBI.
Maombi ni ibada inayokimbiwa makanisani,sababu shida kubwa ya kanisa ni maombi. Ikumbukwe ya kwamba majibu yetu yamefichwa katika maombi. Ukitaka majibu yako,basi omba kwa jina la Yesu Kristo ( Yoh.14:14 )
Maombi ni nguzo kubwa sana katika kanisa,nguzo hii huifanya kanisa kuwa hai. Kanisa lililoegama katika muhimili wa kudumu katika maombi huku likiwa na muongozo wa Roho mtakatifu na neno kwa wingi,basi ujue hakuna pepo,mchawi,wala majini yatakayofanya kazi humo,maana ni lazima maroho hayo yatalambwa kama vile ngo’mbe alambavyo majani.
Biblia inaweka wazi jambo hili;
” Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. ” Mathayo 16:18
Bwana Yesu anamuonesha Petro kwamba kanisa la kweli ni lile lisiloshindwa na milango ya kuzimu,kwa lugha nyingine alikuwa akimwambia kanisa la kweli ni lile linalodumu katika kweli likiomba,sababu yule aliye katika kweli ( neno) akidumu katika kuomba,kamwe hawezi kushindwa na nguvu za malango ya kuzimu.
* Kanisa lisipoomba,kupigwa na adui ni lazima,yafaa nini kuwa mkristo pasipo kuomba! Wachawi,au mapepo katika kanisa hawaogopi chochote kile isipokuwa wanaogopa na kukimbia panapo maombi katika Roho. Maombi katika Roho yana nguvu ya ajabu isiyoweza kuelezeka hapa.
Mambo hayo matatu ni muhimu sana katika kanisa la Kristo Yesu. Na ikiwa waamini watafuata hayo,basi ushindi ni lazima.
FARAJA JUMANNE      KWAYA VIJANA

Tuesday, 28 February 2017

MAMBO YA HUSUYO VIONGOZI KATIKA KANISA

Bwana Yesu asifiwe…

Fundisho hili si la watu wote bali ni la wachache tu hususani wale ambao ni viongozi mbali mbali wa makanisa,fellowship na vikundi mbali mbali vya wokovu. Dhumuni kubwa la fundisho hili ni kukupa maarifa wewe kiongozi kujua nini maana ya uongozi na jinsi ya kuenenda uwapo kanisani.
Ni fundisho lefu sana,lakini ninajaribu kukupa kwa sehemu tu ili usikose maarifa haya. Hivyo tuanze fundisho hili kwa kuangalia wito wa uongozi.

01.WITO WA UONGOZI. (A call to leadership)
Uwezo wa kanisa lolote au organasation yoyote,katika ukuaji unategemea ubora wa uongozi uliopo. Uwezo wa Kanisa letu unategemea na uongozi tuliokuwa nao. “ Uwezo mkubwa ukuaji mkubwa”. Kila kitu kina kuwa na kuanguka kutegemea uwezo wa uongozi uliopo. Kwa maana kila kitu kimejengwa katika uongozi.

~Mara nyingi tunachanganya maana halisi ya uongozi na nafasi ( leadership and position),uongozi sio nafasi kwa sababu kuna kipindi watu wanaweza kuwa na nafasi lakini hawafanyi kazi kama viongozi,lakini tunaweza kuwa na watu wasiokuwa na nafasi lakini ni wachapa kazi kama viongozi.
Tazama;kuna watu wanakuja kanisani wakitazamia wawe viongozi lakini hawana chochote cha kiuongozi. Uongozi hauna uhusiano na nafasi. Uongozi ni uongozi,nafasi ni nafasi.

~ Tena,muda mwingine tunachanganya neno uongozi na umaarufu. Tujue kwamba;uongozi sio umaarufu. Kwa maana mtu anaweza kuwa ni marufu lakini asiwe kiongozi. Tena,uongozi sio kutumia mabavu,(nguvu),kwa maana uongozi hauna uhusiano na nguvu.
Hivyo basi,katika makanisa yetu tuna hali fulani hivi ambayo si nzuri kuhusiana na suala zima la uongozi kwa maana utakuta mchungaji amezungukwa na watu wanaojiita ni viongozi lakini hawajui kitu gani cha kufanya. Viongozi katika kanisa,ni lazima wajue namna ya kuongoza wao wenyewe.

~Changamoto kubwa ya ukuaji wa kanisa iliyopo leo ni suala la uwezo wa uongozi. Ni muhimu kushughulikia suala la uongozi.Tazama; Katika kipindi cha nabii Ezekieli,Waisraeli nao walikuwa wakikumbana na tatizo la uongozi.
Tunasoma; “ Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu. ” Ezekieli 22:30
~Mungu alitafuta mtu mmoja tu atakayesimama kwa ajili ya wengine lakini alikosa. Kwa maneno mengine ni kwamba; Israeli walikuwa na watu wengi wenye nafasi lakini sio viongozi.Kitu kinachowatisha watu wengi ni hali ya kutokukua kiroho.
Wakati unapokuwa hukui wala husogei mbele,mchungaji huogopa hali hiyo lakini hata MUNGU huishangaa hali hiyo isiyokuwa ya kawaida,kwa sababu MUNGU hapendi kukaa bila ukuaji. Ndio maana katika Kumb. 1:6 Neno linasema;

“BWANA, Mungu wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mlivyokaa katika mlima huu vyatosha;” Mungu anataka watu wake waanze kusogea mbele kimaendeleo ya ukuaji na kamwe wasidumae.
Hivyo,kuna kazi kubwa ya kufanya lakini lazima tujue nafasi zetu.
Muda umefika wa kutoshindana sisi kwa sisi katika nyumba ya BWANA wala huu sio muda wa kusengenyana bali ni muda wa kusonga mbele.
Ukisoma katika Mathayo 16:18,biblia inasema;
“Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.” Yesu anasema “Yeye” atalijenga kanisa,sio wewe,bali ni “Yeye” kwa maneno mengi ni Yesu ndiye ajengae kanisa, wajibu wako wewe kama tofali ni kukubali kuwekwa mahali pale Yesu atakapo.

Nami sitakiwi kukataa kuwekwa eneo lolote.Kwa hiyo,Yesu anahitaji kila kiongozi awe na nguvu ya Mungu na kukubali kuwekwa mahali popote pale. Mungu anapokuambia ufanye usafi,basi fanya. Ndani ya nyumba ya Mungu sisi sote tunakuwa ni watoto pasipo kuangalia vyeo vyetu tulivyonavyo.
Sasa,ni majukumu ya viongozi wa kanisa kuanzisha ukuaji na kusimamia ukuaji. Ni jukumu letu kuwapokea wanaokuja,lakini ikiwa watu watakuja na kuondoka ni lazima tujiulize ni kwa sababu gani wameondoka. Ni jukumu letu kuwaonesha upendo na kuwaweka wote hao nyumbani mwa Mungu.
Wala siamini kwamba ukubwa wa mlango ambao watu hutumia kuingia ni sawa na ukumbwa wa mlango wa kutokea.( Kwa maana yapasa mlango wa kuingia uwe mkubwa kuliko wa kutoka) Mungu anataka kuona ukuaji.
~Katika ukuaji wa kanisa,mambo yafuatayo ni mambo muhimu;
01.Mfumo wa ki-Mungu katika ukuaji wa kanisa.
02.Mahusiano kati ya fedha na ukuaji wa kanisa
03.Namna ya kuimarisha na kuwajenga imara watu wanaokuja kanisani kwa mara ya kwanza.
04.Kutengeneza darasa la washirika.

Swali; Kiongozi anazaliwa au anatengenezwa? Je ulizaliwa kuwa kiongozi au ulitengenezwa kuwa kiongozi?

JIBU; Viongozi hawazaliwi kuwa viongozi,bali wanatengenezwa. Kuna watu ambao wanakipawa cha kuwa viongozi lakini kuna watu wengine hawana kipawa na wapo tayari kujifunza. Tabia njema na mtazamo mzuri ni muhimu kwa yeyote anayekuwa kiongozi.

MSINGI WA UONGOZI.
~Msingi wa viongozi wote ni maono,kwa maana hakuna uongozi bila maono.“ Pasipo maono, watu huacha kujizuia;Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.” Mithali 29:18
Maono ni nini? Tafsiri nyepesi ya maono ni kile unachokiona kinachokuja,ni picha au taswira ya mambo yajayo. Kuwa kiongozi ni tofauti na mfanikiwaji. Kiongozi huwa anakuwa na malengo ya kuzidi kuendelea kwa maana hajafanikiwa bado,naye uwahitaji watu kisha na kushirikiana nao katika maono yake. Mungu ametuita kuwa viongozi na si wafanikiwao tu.
Maono yanakujaje?

~Maono yanakuja kutoka katika mzigo. Mungu anaweka mzigo ndani ya mtumishi wake. Kisha Roho mtakatifu anawezesha namna ya kushughulika na huo mzigo na namna ya kumpa taswira hiyo na taswira hiyo inakuwa ni maono. Hivyo hakutakuwa na maono bila mzigo. ~Jukumu la viongozi katika kanisa ni kujua mzigo wa mchungaji wao,kama hatutaelewa mzigo wa mchungaji basi hatutauweza kuubeba.
~Jukumu la mchungaji ni kueleza mzigo wake na maono yake kwa viongozi. Hivyo,mzigo na maono ndio kanisa lenyewe,kwa sababu pale mzigo ulipo ndipo nguvu zetu zipo. Mfano mzigo wetu ni kufundisha neno la Mungu na ndio nguvu yetu ilipo. Watu wakija wakute neno la Mungu kwa sababu ndio mzigo wetu….

FÀRÀJÀ JUMÀNNÈ.... KWAYA YA VIJANA

Friday, 3 February 2017

Tuesday, 27 December 2016

BAADHI YA PICHA ZA UBATIZO SIKU YA JUMATATU TAREHE 26/12/2016

KANISA LA K.K.K.T USHARIKA WA KITUNDA RELINI  Haya ndo baadhi ya matukio ya picha za ubatizo siku ya Jana kama ulikosa picha ya mwanao hizi hapa pia ukihitaji nikusafishie unaweza nijulisha kupitia
0712270303 Faraja jumanne kwaya ya vijana.